• HISTORIA YA KANISA AU UFALME WA MUNGU KATIKA BIBLIA

  NA KITABU CHA INJILI YA FILIPO

  Hello & Welcome!

 • Bofya kitufe cha download hapo juu kupata kitabu cha [PDF]Ufalme Mmoja, Kanisa Moja.

  Bofya kitufe cha submit hapo juu kupata kitabu cha [PDF] Injili ya Filipo

   

  DIBAJI YA KITABU CHA UFALME WA MUNGU

   

  “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalmewako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupeleo riziki yetu ya kila siku, Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. (Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu,hata milele. Amina) [Mt. 6:9-13].” Hii ni sala ijulikanayo kwa jina maarufu la “sala ya Baba yetu”, ambayo watu wengi hupenda kuitumia mara kwa mara; ni sala iliyobeba ujumbe mzito kwa mwombaji, kwa sababu ndio uti wa mgongo wa sala zote waombazo wakristo. Kwa kuwa mada ya kitabu hiki sio sala, bali ni Ufalme wa Mungu; ndio utakaojadiliwa. Katika sala hii ufalme wa Mungu umetajwa mara mbili, ikionyesha umuhimu wa ufalme huo; yaani “Ufalme wako uje na Ufalme ni wako”. Pale wanafunzi wa Yesu Kristo walipoambiwa kuomba kwamba ufalme wa Mungu uje; ulikuwa umekaribia sana na ndio maana mahubiri ya Bwana Yesu na Yohana Mbatizaji yalikuwa yanasisitiza kwamba, watu watubu kwa kuwa Ufalme wa Mungu
  umekaribia. Hivyo maombi juu ya jambo lililotarajiwa, yalikuwa muhimu ili kuweza kuzuia nguvu kinzani juu ya jambo hilo jema. Huu ndio Ufalme ambao wana wa Israeli waliusubiri kwa miaka mingi tangu utabiri wake ulipotolewa na nabii Danieli takribani miaka 500 kabla ya Kristo.

  Muktadha wakitabu hiki ni kuangazia kwa undani namna Ufalme wa Mungu ulivyotabiriwa na
  ambavyo uliwafikia wanadamu wote; ili wote tujue na kuwa na uhakika kwamba
  Ufalme sio kitu cha kusubiri tena, bali kitu cha kuishi ndani yake. Yeyote akipenda
  anaweza kuwa sehemu yake; na kama yeyote atakuwa sehemu yake, atambue kuwa
  Ufalme wa Mungu ni kitu kilichosubiriwa kwa kuanguka na kuinuka kwa wengi kama mzee
  Simeoni mwenye haki alivyosema (Lk.2:25-35). Yeyote hatakiwi kufanya mzaha na Ufalme wa Mungu, ambao kwa sababu yake ililazimu upanga uingie kwenye moyo wa Yesu Kristo, ili fahamu za
  watu wengi ziweze kufunguliwa na kuwa huru. Hakuna awezaye kuwa mtumwa tena baada
  ya kuingia kwenye ushirika wa Ufalme wa Mungu, bali wote huwekwa huru mbali na
  dunia na tamaa zilizomo ndani yake kwa sababu ya mwili (Lk. 4:18-19). Pia utatambua uhusiano uliopo kati ya Ufalme waMungu, Ufalme wa mbinguni na Kanisa katika matumizi yetu leo; yaani kwa nini
  unaitwa Ufalme wa Mungu au Ufalme wa Mbinguni?

  Kabla ya Ufalme wa Mungu, falme nyingi za kidunia zilitokea kama ufalme wa dhahabu,
  ufalme wa fedha, ufalme wa shaba, na ufalme wa chuma na udongo. Utaweza kujua
  falme hizo zote ndani ya kitabu hiki pindi utakapokisoma, lakini lengo kuu
  upate kujua Ufalme wa Mungu; maana Mfalme alipoulizwa kuhusu habari za mamlaka
  yake ya kifalme alisema kuwa, “Ufalmewangu sio wa ulimwengu huu”. Kama Ufalme wake sio wa ulimwengu huu, inamaana hauwezi kufananishwa na falme za ulimwengu huu, japo ukijifunza sifa za Ufalme
  huu utagundua kuwa haujapungukiwa na sifa yoyote ya kuitwa Ufalme, japo una
  sifa za ziada ambazo ni tofauti na zile za falme za kidunia. Kama Ufalme wa
  Mungu ulitegemea wanadamu wawe wakazi wake, na iwapo Ufalme huu sio wa
  ulimwengu huu; je wanadamu hawa, wako katika mwili wa nyama au katika mwili wa
  roho? Kama wanadamu hawa wako katika mwili wa nyama, je inawezekana kuna
  ulimwengu zaidi ya mmoja hapa duniani ambamo watu wanaishi? Kama wanaishi
  katika Roho, hii itakuwa na maana gani iwapo roho haionekani?

   

  Iwapo mtu ataishi kwa tunda la Roho (yaani upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi),
  bila matendo ya mwili (yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima)
  (Gal.5:16-25), je, atakuwa anaishi kwenye mwili au katika Roho? Katika Ufalme wa Mungu, wafu hufufuliwa ili waishi
  katika Roho, sio katika mwili tena; ndio maana wanaweza kuishi kwenye Ufalme wa
  Mungu ambao sio wa ulimwengu huu; kwani wamefufuliwa na kufanyika wakazi wa
  Ufalme wa Mungu; ulimwengu huu kwao, ni ulimwengu mwingine. Hivyo, kuna
  ulimwengu wa waliokufa (yaani watu wasioamini), ulimwengu wa waliofufuliwa (yaani
  walio hai au wanaoamini), pia kuna ulimwengu wa kati wa watu waliopotea (watu
  ambao ni vuguvugu; wanaoigiza kuishi kwa Roho ilhali wanaishi kwenye mwili) (Ufu. 3:15-16). Hata kama Roho haionekani, watu wanaweza kuiishi ili wawe ndani ya Ufalme wa Mungu, na
  wampendeze Mfalme wao. Kuishi katika Roho haimaanishi kwamba mtu hana mwili,
  bali hatawaliwi tena na tamaa za mwili, yaani yuko huru mbali na mwili na
  dunia.

  Mwanzo,kukua na kuenea kwa Ufalme wa Mungu, ni mada itakayoangaziwa katika kitabu
  hiki; yaani, ulianza lini? Ulianzishwa na nani? Ulianzia wapi na ishara ya
  kuanza kwake ni ipi? Je uliweza kukua na kuenea kwa njia gani? Je, bado upo
  duniani hadi leo au ulipita tu? Amebarikiwa kila atakayesoma na kupata majibu
  ya maswali haya yote, maana ataweza kuwa huru na kufanya wengine kuwa huru
  mbali na ufalme wa dunia. “Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?” Pia, “Bali utafuteni kwanza Ufalme wake, nahaki yake; na hayo yote mtazidishiwa”. Maneno haya asingeyasema Mfalme,kama Ufalme wa Mungu usingekuwa jambo kubwa, ambalo yeyote akishindwa kulijua
  na kulipata atapata hasara ya nafsi yake!

  Mungu mbariki, Jovinus Lukonge; Mungu mbariki, David Msaki

   

  Historia ya kanisa katika Biblia

   

  Kanisa lilitabiriwa kwa mara ya kwanza kwa jina la UFALME katika kitabu cha nabii Danieli (Dan. 2:44-45; 7:13-14); kama kitu cha wokovu kwa wanadamu wote duniani; ili kutimiza mpango wa Mungu wa
  wokovu kwa watu wote uliotajwa katika kitabu cha mwanzo (Mw. 3:15). Yeyote anaweza kufahamu kanisa vizuri iwapo atachunguza kwa makini kuanzia kitabu cha Danieli, katika nukuu zilizotajwa hapo chini,
  kama ilivyoandikwa, “Na katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atausimamisha Ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme zote vipande vipande na kuziharibu, nao
  utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile
  dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye;
  na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti” (Dan. 2:44-45); na tena katika (Dan. 7:13-14) twasoma, “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamojana mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye
  akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake
  ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme
  usioweza kuangamizwa”. Wakati nabii Danieli anatoa utabiri, Ufalme huo haukuwepo duniani, bali ulikuwa unatazamiwa kuja katika siku za baadaye.

  Kuna uhusiano kati ya “jiwe lililochongwa kutoka mlimani na mmojaaliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu” yote yakionyesha ujio waMfalme ambaye angetoka juu kupewa Ufalme baada ya kuangamiza falme za kidunia
  zilizowakilishwa na sanamu. Kutoka juu mlimani ni sawa na kuja na mawingu
  ambayo yako juu. Hivyo, kuna uhusiano kati ya ndoto ya mfalme Nebkadreza na
  njozi ya Danieli. Ujio wa Ufalme waMungu unaenda sambamba na ujio wa Mfalme wa Ufalme huo, ili kuangamiza falme za
  kidunia na kusimama milele kama baraka kwa mataifa yote.

  Kabla ya nabii Danieli, taifa la Israeli liliwahi kuwa na ufalme, na wafalme wao wa kidunia ambao walitoka katika kabila ya Yuda, kutokana na baraka za
  Israeli [Yakobo] kabla hajafariki kama ilivyoandikwa, “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba; Kutoka katika
  mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke;
  ni nani atakaye mwamsha? Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya
  sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, ambaye mataifa watamtii. Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya
  zabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa
  maziwa” (Mw.49:8-12).

  Makao makuu ya ufalme wa Israeli yalikuwa Yerusalemu, na wafalme wao walikuwa wana wa Yuda, kuanzia tangu mfalme Daudi na mfalme Suleimani, [isipokuwa Sauli, mfalme wao wa kwanza, aliyetokea kwenye kabila ya Benjamini];
  kabla ya ufalme huo haujagawanyika na kuwa ufalme wa Yuda na ufalme wa Israeli.
  Baadaye, falme hizi mbili zilifanya maovu mbele za Mungu, zikiabudu sanamu na
  kushindwa kushika torati, hadi akaamua kuziangamiza; baada ya kuwapa maonyo ya
  aina mbalimbali kupitia manabii wake bila mafanikio. Ufalme wa Israeli uliangamizwa
  ukiwa wa kwanza, ukifuatiwa na ufalme wa Yuda.

  Kazi ya kuangamiza falme hizi ovu ilifanywa na mfalme Nebkadreza wa taifa la Babiloni. Hivyo, nabii Danieli alipoenda mbele za mfalme Nebkadreza kutoa tafsiri ya ndoto ya mfalme, ilikuwa baada ya maangamizi ya ufalme wa Yuda na
  ufalme wa Israeli, naye alikuwa utumwani nchini Babiloni. Kwa hiyo kuna
  muunganiko wa maana ya ndoto ya mfalme Nebkareza, falme zilizoangamizwa yaani
  [ufalme wa Yuda na ufalme wa Israeli] na Ufalme wa Mungu uliotarajiwa kuja ili
  kuangamiza ufalme wa dhahabu, ufalme wa fedha, ufalme wa shaba na ufalme wa
  chuma na udongo kwa jiwe lililochongwa kutoka mlimani.

  Kutokani na maneno ya unabii ya Yakobo [Israeli] hapo juu, yanaonyeshakuwa ujio wa Mfalme “ambaye mataifa watamtii”, lilikuwa jambo ambalo lina mausiano na uzao wa Yuda. Hivyo jiwe lililochongwa kutoka mlimani, ili kuangamiza sanamu [falme nne za kidunia
  ambazo zingetawala duniani] katika ndoto ya mfalme Nebkadreza, lingetokea
  katika kabila ya Yuda. Hivyo, utabiri wa kuja kwa Ufalme kwa wana wa Israeli
  lilikuwa jambo la faraja sana wakiwa utumwani Babiloni; wakizingatia kuwa
  ufalme wao wa awali uliangamizwa kwa sababu ya kutokutii kwao. Ndio sababu
  baada ya Kristo kufufuka na kukutana wa wanafunzi kabla hajapaa mbinguni,
  walimuuliza swali, “Je! Bwana, wakati huu ndipo utakapowarudishia Israeli ufalme?” kwa sababu walikuwa na shauku kubwa ya kuwa na ufalme wao wenyewe. Shauku hiyo hiyo ya kupata ufalme wao
  tena, iliwafanya wana wa Israeli kumlaki Kristo alipoingia Yerusalemu, wakitandaza
  nguo zao na matawi ya miti na wakisema kuwa, “Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana;Hosana juu mbinguni” (Mt. 21:9). Japo, katika uchambuzi utakaofanyika baadae utadhihirisha namna ambavyo Ufalme wa Mungu ulifanyika
  kanisa la Kristo.

  Kanisa si kitu kilichotokea pasipo mpango; si kitu kilichotokea tu ghafla; bali ni kitu
  kilichotokea kwa mpango maalumu wa Mungu; ambao wale watakaoutafuta, wakauona,
  na kuuamini wataokolewa. Jambo hili ni muhimu sana, kwani ni shida kulitafuta
  na kulifahamu kanisa katika nyakati zetu hizi zenye utitiri wa makanisa,
  yasiyonena mamoja; yaani, yasiyokiri kuwa wanadamu wote wanapaswa kuwa katika
  kanisa moja, na kuwa na imani moja, kama vile Mungu alivyo mmoja (Efe. 4:2-6). Kabla ya kuja Kristo; Mungualinena mambo mengi kupitia manabii (Ebr.1:1), kuhusu kuja kwa Mfalme na Mwokozi wa wanadamu; yaani, kuja kwa Ufalmewa Mungu. Alinena pia kuhusu kuinuka na kuanguka kwa falme kubwa za wanadamu
  kama iliandikwa katika kitabu cha Danieli. Ni vizuri kufahamu uhusiano uliopo,
  kati ya falme za dunia na Ufalme wa Mungu.

   

  Ufalme wa Mungu


  UFALME WA DUNIA UMEKWISHA KUWA UFALME WABWANA WETU NA WA KRISTO WAKE, NAYE ATAMILIKI HATA MILELE NA MILELE [UFU. 11:15].

  Ufalme wa Mungu na Ufalme wa Mbinguni

   

   

  Maneno; Ufalme wa mbinguni na Ufalme wa Mungu, yametumika katika maandiko kwa nyakati
  tofauti. Maneno haya huleta utata kwa wasomaji wa biblia, kama yanamaanisha
  jambo moja au yana maana mbili tofauti. Pakua Kitabu cha ufalme wa mbinguni upate kusoma hayo yote.